DAMU KUTOKA UKENI BAADA YA KUJIFUNGUA
Damu huanza kutoka baada ya kujifungua na kuendelea kwa siku chache .Hujulikana kama lochia na rangi yake hubadilika kadri siku zinavyoenda.
Siku chache za mwanzo huwa damu nyekundu na baada ya siku 4 -5 kubadilika kuwa majimaji zaidi yenye rangi ya kahawia.
Kuanzia kwenyesiku ya 10 na kuendelea huwa na rangi ya njano njano.
Maji maji haya hupungua kadri siku zinavyoenda na kuisha ndani ya wiki 6 baada ya kujifungua. Baadhi ya wanawake inaweza kutokea yakaendelea mpaka wiki ya 8.
Katika kipindi hiki kuwa makini kutazama kiasi cha damu kinachotoka, hasa pale unapobadilidha pamba au pedi ikiwa imeloa damu sana au maji yakiwa na harufu mbaya. Onana na daktari wako ikiwa hayo yanatokea.
No comments:
Post a Comment