Search your Topic here

Sunday, June 12, 2016

MADHARA YA UTUMIAJI WA COCAINE NA HEROIN

Cocaine
Hutokana na majani ya mmea uitwao kitaalamu Erythroxylum coca bush.
Aina hii ya dawa ya kulevya hutolewa
kwa mifumo ifuatayo;
Unga ambapo mitaani hujulikana
kama ‘coke’ na hutumika kwa
kuvutwa puani kama unga, au
kuyeyushwa na maji na kuchomwa
kwenye mshipa wa damu.
Crack ambapo mitaani hujulikana
kwa jina hilohilo crack au rock, na
hutengenezwa kwa kuchanganywa
na kemikali. Na hutumika kwa
kuvutwa kama sigara.
Cocaine pindi inapoingia kwenye damu huenda kwenye ubongo na kuzuia ufyonzwaji wa vihisishi vifuatavyo:
Dopamine, norepinephrine na serotonin,
kutoka kwenye ubongo. Hivyo ubakia
kwenye ubongo. Na vihisishi hivi
husababisha ile hali ya furaha,
mchangamfu na kujisikia mwenye nguvu kitaalamu euphoria. Na huweza kuwa kwenye hali hii kwa nusu saa tu.
Mara tu baada kutumia dawa hii dalili
zifuatazo hutokea
Mishipa ya damu husinyaa (constricted blood vessels)
Joto la mwili huongezeka
Mapigo ya moyo huongezeka
Shinikizo la damu
Dilated pupils
Matumizi ya muda mrefu ya dawa hii ya kulevya huleta madhara yafuatayo; Pamoja na kwenda kwenye ubongo husambaa
sehemu nyingine za mwili na mzunguko wa damu
1. Moyo - Kwenye moyo huweza
kuleta Shambulizi la moyo (heart
attack) na vilevile mapigo ya moyo
yasiyo na mpangilio (Arrhythmia)
hivyo unaweza kufa ghafla tu.
2. Ubongo - Mishipa ya damu kwenye
ubongo inaweza kusinyaa na
kupelekea kupata Kiharusi, hata
kwa kijana. Vilevile unaweza
kupata ugonjwa wa akili (substance
abuse pyschosis).
3. Mapafu na mfumo wa hewa -
Uvutaji kupitia pua huweza
kupelekea tatizo sugu la kutokwa
damu puani kila wakati na mafua
yasiyo pona, kupoteza mfumo wa
harufu, na ikivutwa kama sigara
kuharibu mapafu moja kwa moja.
4. Mfumo wa chakula - Cocaine
husababisha kusinyaa kwa mishipa
ya damu kwenye tumbo na utumbo
hivyo kusababisha vidonda na
kuweza kuharibu kabisa mfumo
huu kwa utumbo kuoza.
5. Mafigo - kutokana na shinikizo la
damu mafigo yanaweza kushindwa
kufanya kazi vizuri, vilevile
cocaine inaweza kuleta madahara
moja kwa moja kwenye mafigo
kitaalamu Rhabdomyolysis.
6. Ngono - ingawa cocaine huweza
kutumika kama njia ya kuongeza
hamu ya ngono huweza
kusababisha kushindwa kumaliza
kile ulichokianza. Matumizi sugu
ya dawa hii ya kulevya huleta
madhara kwa jinsia zote yani kwa
wanaume na wanawake.
7. Na vilevile huweza kufanya kuwa
tegemezi wa dawa hii.
8. Kwa wanaotumia sindano na
kushea wanaweza kupata
maambukizi ya virusi ya hepatitis
na vya ukimwi.
Nini hutokea baada ya matumizi ya muda mrefu ya kokeni?
Baada ya kutumia cocaine kwa muda mrefu punde unapoacha tu kutumia dalili zifuatazo hutokea;
Uchovu
Kushindwa kuzingatia na kutokuwa makini
Kukosa uwezo wa kuwa na furaha
au kusikia raha
Kuongezeka kwa tama zaidi ya
kutumia cocaine
Kujisikia kuumwa, maumivu,
baridi na kutetemeka.
Ikitokea mtu akitumia zaidi ya kiwango kinachotakiwa kwa muda mfupi yaani overdose, kifo cha ghafla huweza kutokea kutokana na madhara yafuatayo;
Moyo kushindwa kufanya kazi
Kiharusi
Degedege mara kwa mara
Mfumo wa hewa kushindwa
kufanya kazi
Heroin
Hujulikana vilevile kama diamorphine,
hutokana na mmea huitwao kitaalamu opium poppy.
     Heroin kwa mfumo wa
Morphine hutumiwa hospitalini kama
dawa ya maumivu makali ya ghafla (acute pain) kwenye maumivu makali ya kifua wakati wa shambulizi la moyo, na kwa maumivu ya mtu aliyepata ajali, vilevile baada ya upasuaji, na maumivu sugu
kwenye kansa.
Hivyo hutolewa kwa kuangalifu mkubwa. Aina hii ya dawa ya kulevya huweza kutumika kwa kuvuta kwa pua, kuvuta kama sigara na kwa kuchoma kwenye mshipa.
Siku hizi watu hutumia njia ya haja kubwa na kwenye uke, ambapo kuta
hufyonza heroin na kuanza kufanya kazi ndani ya sekunde arobaini.
Heroin mara tu baada ya kuingia kwenye damu kuenda kwenye mfumo wa neva na kukandamiza ufanyaji kazi wake, ndio huweza kutumika kupunguza maumivu.
Dalili za mtu aliyetumia heroin
Dalili ambazo hutokea mara tu
anapotumia Heroin:
Kujisikia mwenye furaha na raha
Kupishana Kusikia hali usingizi na
tahadhari
Midomo kuwa mikavu
Misuli kuishiwa nguvu
Kuhema polepole
Warm skin flushing
Mikono na miguu kuwa mizito
kope za macho kulegea
Nini madhara ya matumizi ya muda
mrefu ya heroin?
Madhara ya matumizi ya muda mrefu wa dawa hii ya kulevya hutokana zaidi na matumizi ya sindano na vifaa vingine visivyo salama
Maambukizi kwenye kuta na
milango ya moyo
Maambukizi ya ini na virusi (kama
hepatitis C na HIV),
Maambukizi ya figo
Maambukizi ya mfumo wa hewa
Maambukizi ya ngozi na majipu
Dalili ambazo hutokea mara tu
unapoacha kutumia heroin;
Kutotulia
Maumivu ya misuli na mifupa
Kutapika
Dalili hizi hufikia kilele ndani ya
masaa 48 hadi 72 na hufika
kikomo baada ya wiki

No comments:

Follow us