Hatua za Ujauzito: Nini Hutokea kwa watoto wachanga na wajawazito Kila Mwezi

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Dalili za kwanza za ujauzito zinaweza kuwa tofauti kutoka kwa mtu hadi mtu.

Kwa sehemu kubwa, ugunduzi hufanywa ndani ya mwezi wa kwanza, si kwa ishara maalum, lakini kwa kutambua kwamba siku zako za mwezi zimechelewa, uthibitisho huja baada ya kipimo kuonesha kuwa una ujauzito.

Ili kutengenza kiumbe kipya, hakuna shaka kwamba mwili na akili hupitia mabadiliko mengi ambayo hukua kutoka kwa kiumbe chenye seli moja hadi mtoto aliyekamilika kabisa, tayari kuishi nje ya tumbo la mama.

Kila hatua ya ujauzito huleta hisia tofauti na mabadiliko, na inaweza kuwa ya kutisha haswa kwa mama na baba wa mara ya kwanza, kujaribu kujua ni nini kawaida na kipi sio kaaida.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni muhimu kukumbuka kwamba, ingawa inatarajiwa, unaweza usipate dalili zote zilizoelezwa katika ripoti kila mwili hupokea mabadiliko hayo tofauti. Cha muhimu kudumisha mazungumzo ya mara kwa mara na daktari wako na kushauriana naye ikiwa kuna shaka.

Trimester ya kwanza (Miezi mitatu ya kwanza)

Mwezi wa 1 (wiki 1 hadi 4)

Wakati wa kwenda kwenye matibabu kwa mara ya kwanza, ni kawaida kwa mtaalamu wa afya kukuuliza maswali mengi kuhusu historia ya matibabu ya familia yako.

Uchunguzi wa ndani wa nyonga pia hufanywa ili kuangalia uterasi, uke na mlango wa uzazi na uchunguzi wa pap (kwa ajili ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi) unaweza kuombwa ikiwa mjamzito haijafanyiwa kipindi cha karibuni, ndani ya mwaka mmoja.

Vipimo vya kawaida vya damu na mkojo pia hufanyika kwa mara hii ya kwanza, pamoja na ukaguzi wa jumla wa afya, ikiwa ni pamoja na urefu, uzito na shinikizo la damu.

Vitamini na folic acid, ambayo huchangia malezi sahihi ya mtoto, inashauriwa kwa wanawake wajawazito katika awamu hii ya awali.

Kwa sababu za usalama, ni muhimu kushirikisha habari kuhusu dawa au virutubisho vyovyote unavyotumia na daktari.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Uzalishaji wa homoni wakati wa ujauzito, ambayo huanza mwezi wa kwanza, ni jambo gumu sana, anaelezea Rodrigo Buzzini, daktari wa wanawake na daktari wa uzazi na mkurugenzi wa kikundi cha Santa Joana.

"Uzalishaji wa homoni, hasa HCG [ambayo hutumika kama kiashiria cha ujauzito], ni mkali sana. Kuwa na kiashiria mwanzoni, viwango vinaongezeka mara mbili kila saa 48 na kuendelea kuongezeka hadi wiki ya kumi na mbili. ", anaelezea mtaalamu.

Mabadiliko haya yanaweza kusababisha kusinzia, kichefuchefu na kumfanya mtu kutaka kujitenga zaidi bila kushiriki kufanya shughuli nyingi.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

"Lakini hii inategemeana na mtu, kwa kuzingatia mazingira yao ya kibaolojia na kisaikolojia", anabainisha daktari.

Watu wengine pia hupata mabadiliko katika hamu ya kula ambayo inaweza kujumuisha kuongezeka kwa njaa lakini pia kuchukia chakula.

Hata hivyo ni muhimu, kwa mujibu wa madaktari, mwanamke mjamzito anatakiwa kuendelea kula kawaida, sawa na mtu ambaye si mjamzito, lakini kwa kuzingatia kwamba mtoto atapata madhara chanya au hasi kulingana nguvu ya mama.

Ukuaji wa mtoto

Katika hatua hii, kijusi kina kinakuwa na urefu wa milimita 0.1 hadi 0.2 tu na kinaitwa blastocyst. Katika wiki tatu za ujauzito, Jenetiki za maumbile tayari zimetengenezwa na jinsia inakuwa tayari ingawa haiwezekani kutambua kwa uchunguzi wa matibabu.

Mwezi wa 2 (wiki 5 hadi 8)

Ikiwa hii ni maya yako ya kwanza kwa daktari, baadhi ya wanawake hawatambui mimba katika mwezi wa kwanza utatakiwa kufanya vipimo vilivyotajwa.

Uzito wako na shinikizo la damu pia vitapimwa na kufuatiliwa. "Katika wiki ya sita, tayari inawezekana kufanya uchunguzi wa ultrasound ya uke, ambayo ni, kuona mfuko wa ujauzito na kutathmini miundo inayoonyesha kama ujauzito unaendelea vizuri," anaelezea Ellen Freire, daktari wa magonjwa ya wanawake na uzazi.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Kwa mujibu wa Freire, mwanamke hawezi kujisikia chochote, lakini kwa baadhi ya wanawake wengine wajawazito, awamu hii dalili za "kawaida" za ujauzito huongezeka.

"Wanaweza kuonesha kwa kushuka kwa shinikizo, kichefuchefu mara kwa mara na kutapika. Tunapendekeza kuchukua tahadhari zaidi na chakula na sio kujitibu."

Ukuaji wa mtoto

"Kati ya wiki tano na sita, 'mbegu' ndogo tayari ina urefu wa milimita tano. Baadhi ya wanawake wajawazito wanashangaa jinsi mabadiliko madogo yanaweza kuwa na athari inayoonekana, ni kwa sababu mwili umeingia katika hali ya ujauzito," anafafanua daktari.

Vipengele vinaendelea kuundwa, kama vile vidole na macho, mrija wa neva, muundo wa kiinitete ambao utatoa ubongo na uti wa mgongo, tayari umeundwa vizuri sasa. Njia ya utumbo na viungo vya hisia pia huanza kujitengeneza. Kuanzia wiki ya sita, kiini cha moyo huanza kudunda. Tunaweza kusikia kwenye ultrasound na ni wakati wa kihisia sana, kawaida ndio wakati wazazi "wanaona mwanga".

 Mbali na kuwa raha kwa wanandoa, ni ishara ya ujauzito mzuri”, anasisitiza Bw. Freire.

Mwezi wa 3 (wiki 9 hadi 12)

Ni wakati wa kurudi kwa daktari, ambapo daktari atasikiliza malalamiko yoyote na kujibu maswali ya mwanamke mjamzito.

"Tunaomba uchunguzi wa ultrasound wa trimester ya kwanza ambayo inatuonyesha maelezo muhimu sana ya kijusi kuhusiana na placenta, sura na ukuaji wa mtoto ambao lazima uwe umekuwa mara mbili ya ultrasound ya kwanza na tathmini ya hatari ya dalili za magonjwa hufanyika", anaelezea Buzzini.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Matiti ya mwanamke mjamzito huongezeka na chuchu huwa nyeusi na kwa wanawake wengine, chunusi zinaweza kutokea. hamu ya kula inaweza kuanza kurudi na kwa mara ya kwanza "njaa ya ujauzito" huanza kujitokeza.

"Tumbo pia huanza kuonekana na ni vigumu kutotambua ujauzito," anasema Freire. Ukuaji wa mtoto

Mwishoni mwa mwezi wa tatu, kijusi huwa na urefu wa sentimita 10 na kawaida huwa na uzito wa gramu 28. Mikono, viganja, vidole, vidole vya mguuni na vidole gumba tayari vimeundwa kikamilifu. kucha huonekana na meno huanza kuundwa chini ya ufizi. Katika awamu hii, kijusi huanza kuzunguka katika mazingira yake kidogo, kufanya mambo kama kufungua ngumi na mdomo.

Trimester ya pili (Miezi mitatu ya pili)

Mwezi wa 4 (wiki 13 hadi 16)

Mama mtarajiwa yuko karibu nusu ya ujauzito wake.

Kipindi hiki ni hatua muhimu ya ujauzito, inawezekana kujua jinsia ya kibiolojia ya mtoto kwa msaada wa ultrasound.

Kutokana na maendeleo makubwa ya kijusi, nafasi za kuharibika kwa mimba hupungua kwa kiasi kikubwa.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Moyo wa mama husukuma damu haraka ili kumtia nguvu yeye na mwili wa mtoto, hivyo dalili kama vile kizunguzungu na kushindwa kupumua vizuri ni kawaida.

Anaweza pia kuteseka na kukosa choo na maumivu ya mgongo kutokana na ukuaji wa mtoto

Ukuaji wa mtoto

"Viungo vinakaribia kutengenezwa kikamilifu na mapigo wa moyo wa kiumbe sasa unaweza kusikika kwa kutumia kifaa kinachoitwa doppler," asema Bi Buzzini.

Kope, nyusi, kucha na nywele huonekana. Meno na mifupa kuwa mnene.

Mtoto tayari anaweza kufanya vitendo kama vile kunyonya kidole gumba, kupiga miayo, kunyoosha na kutengeneza nyuso za kuchekesha.

Mfumo wa neva huanza kufanya kazi polepole. "Viungo vya uzazi tayari vimeundwa, kwa hiyo, kulingana na nafasi ya mtoto kwenye ultrasound, tayari inawezekana kugundua jinsia. Mtoto pia anapata hisia iwezekanavyo kwa mwanga na sauti ", inabainisha daktari wa wanawake.

DDD

Chanzo cha picha, Getty Images








Mwezi wa 5 (wiki 17 hadi 20)

Mwishoni mwa mwezi wa tano, mwanamke mjamzito hufanyiwa uchunguzi wa pili wa maumbile ambao ni muhimu kama wa kwanza katika kutathmini ukuaji sahihi wa mtoto tumboni.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Wanawake wengi huongezeka kati ya pauni 2.5 na 6.5 kwa wakati huu na mfuko wa uzazi unakuwa na ukubwa wa tikiti. Kwa kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo, kitovu kinaweza kutokea nje.

Hamu ya kula inaweza kuongezeka na baadhi ya wanawake wanakabiliwa na kupoteza kumbukumbu, inayoitwa "pregnancy brain" kwa Kiingereza. Katika awamu hii, wanawake wajawazito wanaweza kuwa na ugumu wa kukumbuka maelezo au kuwa makini na kazi.

Ukuaji wa mtoto

"Mtoto tayari anaweza kuhisi na kusikia, kwa hivyo tunapendekeza kusikiliza muziki na kuzungumza ili kufanya mazingira ya nje ya mfuko wa uzazi kuingiliana," anatoa maoni Buzzini.

Wakati wa ultrasound, mtaalamu huangalia viungo kwa kina vya moyo, kibofu, figo na vingine na kuhesabu vidole vya mtoto ambavyo vinaweza kusogea na mama akahisi kucheza.

Mwezi wa 6 (wiki 21 hadi 24)

"Mwanamke mjamzito anapokaribia mwisho wa miezi mitatu ya pili ya ujauzito, ni muhimu kumsikiliza ili asihisi kuzidiwa," alisema Bi Buzzini.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

"Imethibitishwa kuwa kuna mzunguko mkubwa wa shinikizo la damu na shida ya tezi katika hatua hii kwa hivyo tunafanya uchunguzi," anasema daktari.

Wanawake wengi pia hupimwa kisukari cha ujauzito, ugonjwa unaosababishwa na kuongezeka kwa upinzani wa insulini kutokana na homoni za ujauzito.

Ukuaji wa mtoto

Katika mfuko wa uzazi, kupima moyo wa mtoto, ultrasound maalum ya moyo wa kijusi, hufanywa. Mtoto tayari ana uzito zaidi ya kilo na kucheza kwake kawaida huhisiwa zaidi na mwanamke mjamzito.

ggg

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwezi wa 7 (wiki 25 hadi 28)

Majadiliano yanafanyika kati ya wanawake wajawazito na wataalamu wa afya kuhusu upangaji uzazi na ishara za tahadhari.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Kijusi kikiwa na uzani wa kilo moja, mama tayari ana uzito zaidi na anaweza kuhisi uchovu.

"Wagonjwa wengine wanasema wanahisi tumbo lao likitikisika. Ni mtoto kuwa na kwikwi na ni kawaida kabisa," Rodrigo Buzzini asema.

Ukuaji wa mtoto

Kijusi kinaendelea kukomaa na kuendeleza hifadhi ya mafuta mwilini. Maji maji ya amniotic huanza kupungua. Katika kesi za kuzaliwa mtoto kabla ya wakati, nafasi ya mtoto ya kuishi huongezeka baada ya mwezi wa saba.

Trimester ya tatu (Miezi mitatu ya mwisho)

Mwezi wa 8 (wiki 29 hadi 32)

Familia huanza kuhesabu hadi kuwasili kwa mtoto huku mwanamke mjamzito akifanyiwa uchunguzi wa kawaida kama vile vipimo vya damu na mkojo, kupima uzito na shinikizo la damu.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Mama anaendelea kuongeza nusu kilo kwa wiki na anaweza kuhisi usumbufu wakati mtoto anaposogea. Kwa kuwa mtoto tayari anaweza kuwa na uzito wa kilo mbili, inawezekana kwamba kucheza kwake kunaweza kukusababishi usumbufu kwenye mbavu za mwanamke mjamzito. Anaweza hata kuacha kuendelea na shughuli za kila siku na kuwa mwangalifu zaidi.

Ukuaji wa mtoto

Mapafu na mfumo wa neva ziko katika awamu ya mwisho ya kukomaa na hatari kubwa ya kuzaliwa kabla ya wakati haipo tena.

Miezi 9 na 10 (wiki 33 hadi 40)

Mashauriano na daktari huwa ya wiki mbili au wiki. Mimba inaweza kuingia mwezi wa kumi lakini baada ya wiki 37 mtoto tayari ameundwa vizuri na hafikiriwi tena kuwa mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati.

Katika awamu hii ya mwisho, madaktari huagiza vipimo ili kujiandaa kwa wakati wa kujifungua.

Kwa nini wanawake wajawazito wana hamu ya kula? Damu na mkojo hupimwa na kuangaliwa ili kubaini kisababishi kikuu cha awali cha ugonjwa wa sepsis (tatizo la kuambukiza linalohatarisha maisha) kwa watoto wachanga.

Ikiwa ni matakwa ya mwanamke mjamzito, mtaalamu wa afya hutathmini uwezekano wa kuzaa kwa kawaida lakini tathmini sio ya uhakika, kunaweza kuwa na mabadiliko baada ya muda, siku ya kuwasili kwa mtoto.

Mabadiliko kwa mwanamke mjamzito

Mtoto anaposogea hadi katika nafasi nzuri zaidi ya kujifungua, mama anaweza kuhisi unafuu kutokana na mgandamizo wa viungo na kupumua kwa urahisi zaidi.

Ukuaji wa mtoto

Mapafu ya mtoto yapo katika hatua za mwisho za kukomaa na tayari ubongo umekua sana na tayari kuanza kupokea vichocheo kutoka kwa ulimwengu wa nje. Mtoto huzaliwa na urefu wa takriban sentimita 50 na anaweza kuwa na uzito kati ya kilo 2.5 na 4.